Ulimwengu

Marekani na Iran waendelea kubwatukiana katikati ya maandamano na vurugu

Maandamano yameharibu miundombinu na nyumba za ibada.

Newstimehub

Newstimehub

14 Januari, 2026

270

Maandamano makubwa nchini Iran yamezua tafrani, yakisababisha uharibifu wa miundombinu, ofisi za serikali na hata nyumba za ibada. Serikali ya Iran inadai maandamano hayo yamechochewa na Marekani na Israel, huku ikiwakejeli waandamanaji kwa “kumfurahisha Rais Donald Trump.”

Pamoja na msako mkali wa vyombo vya usalama, kumekuwepo pia maandamano ya kuunga mkono serikali. Marekani na Israel wanayafuatilia kwa karibu, wakitaka kujua iwapo vurugu hizi zinaweza kuathiri utawala wa Kiislamu wa Iran, ambao mara kwa mara umekuwa ukihusishwa na tishio la nyuklia.

Waandamanaji wengine wameomba msaada wa Trump, naye akaitahadharisha Iran dhidi ya kutumia nguvu kupita kiasi. Hali hii imeongeza wasiwasi katika kanda, hasa ikizingatiwa nafasi ya Iran kama mzalishaji mkubwa wa mafuta.

Iran imesema iwapo itashambuliwa na Marekani, itajibu kwa kushambulia kambi za Marekani katika eneo hilo. Kwa sasa, hali imebaki kuwa vita vya maneno, kila upande ukionyesha msimamo mkali huku ukitafakari hatua inayofuata.

CHANZO: TRT Afrika