Kenya imefikia makubaliano ya awali ya kibiashara na China ambayo yanaruhusu asilimia 98.2 ya bidhaa zake za kuuza nje kuingia kwenye soko la China bila ushuru. Wizara ya Biashara ya Kenya imesema Alhamisi kuwa mazungumzo hayo ni hatua ya mwanzo kuelekea makubaliano kamili ya pande mbili.
Rais William Ruto alifanya ziara ya kitaifa Beijing mwaka jana ambapo alisaini mikataba kadhaa ya ufadhili na ushirikiano, hatua iliyodhihirisha kuimarika kwa uhusiano wa Nairobi na Beijing. Ruto ametetea msimamo huo licha ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya maafisa wa Marekani, akisisitiza kuwa Kenya inalazimika kuongeza mauzo yake kwa China ili kupunguza pengo kubwa la kibiashara linaloinufaisha Beijing.
CHANZO: TRT Afrika














