Afrika

ACT-Wazalendo yalaani hatua ya ZEC kuteketeza nyaraka za uchaguzi

ACT-Wazalendo: kuteketeza nyaraka ni uhujumu wa ushahidi.

Newstimehub

Newstimehub

4 Februari, 2026

843828d751573d7c87f04e720428967b5c439b013198903bb76cf41e31a2dfc7

Chama cha ACT-Wazalendo kimepinga vikali uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wa kuchoma nyaraka za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Katika taarifa yake ya Februari 4, 2026, chama hicho kimesema kuwa kucheleweshwa kwa maombi yake ya Mahakama kuwasilisha nyaraka hizo ni mkakati wa makusudi wa kuzuia haki na kutoa nafasi kwa ZEC kuharibu ushahidi.

ACT-Wazalendo kimesisitiza kuwa ni kosa la jinai kuharibu nyaraka wakati kesi za kisheria bado zinaendelea, na kwamba kitendo hicho ni dharau kwa Mahakama.

Kwa upande wake, ZEC imesema zoezi hilo limeidhinishwa Februari 3, 2026 kwa mujibu wa kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, kinachoelekeza nyaraka zote za uchaguzi kuteketezwa baada ya siku 90 tangu kumalizika kwa uchaguzi.

CHANZO: TRT Afrika