Ndege kadhaa za kivita za Marekani zimeanguka nchini Kuwait Jumatatu asubuhi, lakini wahudumu wote waliokuwa ndani waliokolewa wakiwa hai, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Kuwait.
Mamlaka zilisema timu za uokoaji zilifika haraka eneo la tukio na kuwapeleka wahudumu hospitalini kwa matibabu, huku hali zao zikielezwa kuwa nzuri. Uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Tukio hilo limetokea wakati mvutano ukiendelea katika eneo la Ghuba huku mashambulizi yakiripotiwa kuendelea kwa siku ya tatu mfululizo.
CHANZO: TRT Afrika














