Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati umeanza kuathiri uchumi wa nchi, ukipelekea kupanda kwa bei ya mafuta kwa takriban asilimia 13. Rais ameeleza kuwa iwapo hali hii itaendelea, inaweza kuathiri uchumi wa Taifa na maisha ya wananchi.
Kauli hii ilitolewa wakati Rais akizindua mradi wa ujenzi wa matanki ya kuhifadhi mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, mradi unaolenga kuongeza uwezo wa uhifadhi wa nishati na kufanya jiji hilo kuwa kitovu cha biashara ya mafuta Afrika Mashariki.
CHANZO: TRT Afrika














