Wakimbizi 74 wa Burundi waliokuwa wakiishi nchini Rwanda wamerejea nchini mwao kupitia mpaka wa Nemba ulioko wilaya ya Busegera.
Kundi hilo lilihusisha wakimbizi 62 waliokuwa wakiishi katika kambi ya Mahama Refugee Camp pamoja na wengine 12 kutoka jiji la Kigali.
Kwa mujibu wa mamlaka za Rwanda, zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa hiari wa kuwarejesha wakimbizi nchini Burundi chini ya uratibu wa serikali na wadau wa kimataifa.
Tangu mwaka 2020, zaidi ya wakimbizi 31,000 wa Burundi wamewezeshwa kurejea nyumbani kupitia mpango huo.
CHANZO: TRT Afrika














