Serikali ya Kenya imemtangaza Jaji wa Mahakama ya Juu, Njoki Ndung’u, kuwa mgombea wa nafasi ya jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Uteuzi huo ulifanywa na Rais William Ruto, ambaye alieleza kuwa Ndung’u ana uzoefu mkubwa katika sheria na masuala ya utawala bora.
Uchaguzi wa majaji wa ICC unatarajiwa kufanyika wakati wa kikao cha 25 cha Bunge la Nchi Wanachama kitakachofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kuanzia tarehe 7 hadi 17 Desemba 2026.
Katika uchaguzi huo, majaji sita watachaguliwa kujiunga na mahakama hiyo ya kimataifa inayosimamia kesi za uhalifu mkubwa kama mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita.
CHANZO: TRT Afrika














