Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameongoza hafla ya kitaifa ya kuzika upya mabaki ya watu 63 waliorejeshwa kutoka Ulaya, ambako yalikuwa yamehifadhiwa kwa miaka mingi katika makumbusho.
Serikali imeeleza kuwa mabaki hayo yalichukuliwa kinyume cha sheria wakati wa ukoloni, yakitoka katika jamii za asili za Khoi na San. Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kurejesha utu na heshima ya wahanga wa historia ya ukoloni.
CHANZO: TRT Afrika














