Usalama Afrika

Nigeria Yapanga Kuwarejesha Raia Wake Wanaotaka Kuondoka Afrika Kusini Kufuatia Mashambulizi.

Serikali ya Nigeria imetangaza mpango wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko Afrika Kusini ambao wako tayari kuondoka baada ya kushuhudia mashambulizi dhidi ya wageni.

Newstimehub

Newstimehub

4 Mei, 2026

2a8f46f0 4798 11f1 bd52 e755d604ece4.jpg

Serikali ya Nigeria imetangaza rasmi kuwa imeanza maandalizi ya kuwarejesha nchini humo raia wake walioko Afrika Kusini ambao wanahofia usalama wao kufuatia ongezeko la mashambulizi yanayolenga wageni,Hatua hiyo imekuja baada ya matukio kadhaa ya vurugu kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya Afrika Kusini, ambapo wahamiaji na wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika, ikiwemo Nigeria, wamekuwa wakilengwa na kushambuliwa.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Nigeria, mpango huo utawahusu wale wote watakaoonyesha nia ya kurejea nyumbani kwa hiari, huku serikali ikiahidi kushirikiana na mamlaka za Afrika Kusini ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa usalama na utaratibu mzuri,

Mashambulizi hayo yamezua hofu kubwa miongoni mwa jamii ya Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini, wengi wao wakieleza wasiwasi juu ya usalama wa maisha na biashara zao. Baadhi yao tayari wameanza kufunga shughuli zao wakisubiri msaada wa kurejeshwa nyumbani.

Wachambuzi wa masuala ya kijamii wanasema hali hiyo inaonyesha changamoto kubwa ya chuki dhidi ya wageni (xenophobia) ambayo imekuwa ikijirudia nchini Afrika Kusini kwa miaka kadhaa sasa, Wanasisitiza umuhimu wa hatua madhubuti za serikali ya Afrika Kusini kulinda haki na usalama wa watu wote wanaoishi nchini humo bila kujali uraia wao.

Aidha, serikali ya Nigeria imewataka raia wake kubaki watulivu huku ikiendelea kufuatilia kwo’ ibu maendeleo ya hali hiyo na kuhakikisha usalama wapewa kipaumbele.

Chanzo:Africanews