Afrika

Tanzania yasukuma matumizi ya Akili Mnemba kuharakisha maendeleo EAC

Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa AI katika kukuza maendeleo ya sekta mbalimbali ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Newstimehub

Newstimehub

1 Aprili, 2026

601

Serikali ya Tanzania imesisitiza matumizi ya Akili Mnemba (AI) kama nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Wito huo umetolewa na Mahmoud Thabit Kombo wakati wa Kongamano la Nne la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu lililofanyika Kigali, Rwanda.

Amesema AI inaweza kuongeza tija katika sekta muhimu kama kilimo, afya, elimu, viwanda na biashara, huku ikiboresha utoaji wa huduma za umma na ushindani wa kiuchumi.

Kongamano hilo limewakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu na wadau wa maendeleo kujadili namna ya kutumia teknolojia kuimarisha ukuaji wa uchumi wa kikanda.

CHANZO: TRT Afrika