Uchumi Afrika

Waagizaji wasitisha manunuzi ya madini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Hatua hiyo yafuatia changamoto za usafirishaji kupitia Mashariki ya Kati.

Newstimehub

Newstimehub

14 Aprili, 2026

617

Waagizaji wa madini ya shaba na kobalti kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesitisha manunuzi yao mwezi huu, kufuatia usumbufu mkubwa wa usafirishaji kupitia Mashariki ya Kati.

Vyanzo vya sekta hiyo vimeiambia Reuters kuwa hali hiyo imeathiri mwenendo wa biashara ya kimataifa ya madini, huku baadhi ya mizigo ikisitishwa licha ya mikataba kusainiwa mapema mwezi Aprili.

Hatua hiyo inaongeza presha katika soko la kimataifa la malighafi muhimu kwa viwanda vya teknolojia na nishati safi.

CHANZO: TRT Afrika