Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu mteule wa Hungary Péter Magyar kuhusu kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, Erdogan alisema kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Hungary umejengwa juu ya historia na utamaduni wa pamoja.
Alisisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuimarika katika siku zijazo kupitia majukwaa ya kimataifa na ya nchi mbili.
CHANZO: TRT Afrika














