Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kupokea dozi milioni 2 za chanjo ya ugonjwa wa mguu na midomo kutoka Uturuki, kama sehemu ya juhudi za kudhibiti mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo.
Chanjo hiyo imetolewa na kampuni ya Dollvet na itasambazwa kwa majimbo kulingana na idadi ya mifugo na kiwango cha hatari.
Ugonjwa wa Mguu na Midomo ni maambukizi hatari yanayoathiri ng’ombe, yakisababisha maumivu na kupungua kwa uzalishaji wa mifugo.
Serikali pia imeagiza dozi nyingine milioni 4 kutoka kwa Dollvet ili kuongeza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo.
CHANZO: TRT Afrika














