Serikali ya Zambia imethibitisha kuwa imechukua mwili wa rais wa zamani Edgar Lungu huku mvutano ukiendelea kati yake na familia ya marehemu kuhusu namna ya mazishi.
Lungu alifariki miezi 10 iliyopita nchini Afrika Kusini, na serikali inasisitiza kuwa anastahili kuzikwa kwa heshima za kitaifa jijini Lusaka, katika eneo maalum la viongozi wa kitaifa.
Hata hivyo, familia ya marehemu imepinga hatua hiyo, ikitaka mazishi ya faragha ya kifamilia badala ya yale ya kitaifa.
Mahakama ya Afrika Kusini awali iliruhusu kurejeshwa kwa mwili huo nchini Zambia, lakini tofauti za maoni zimeendelea kuhusu utaratibu wa mazishi.
CHANZO: TRT Afrika














