Rais wa Kenya William Ruto ametangaza mabadiliko makubwa ya sera ya rasilimali kwa kusema kuwa Kenya haitasafirisha tena madini ghafi nje ya nchi.
Akizungumza katika kongamano la “Afrika We Build” jijini Nairobi, Ruto alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya rasilimali za taifa, kukuza viwanda vya ndani na kuimarisha ajira kwa wananchi.
Alisisitiza kuwa kwa miaka mingi Kenya imekuwa ikipoteza mapato na fursa za kiuchumi kwa kusafirisha malighafi bila kuzichakata, akitoa mfano wa kampuni ya Base Titanium ambayo ilisafirisha madini bila faida kubwa kwa taifa.
Ruto aliongeza kuwa serikali itawekeza katika miundombinu ya viwanda, kuvutia wawekezaji na kuimarisha sera zitakazosaidia usindikaji wa madini ndani ya nchi.
















