Kemi Seba ni mwanaharakati maarufu wa Pan-African anayejulikana kwa kupinga ushawishi wa nchi za Magharibi, hasa Ufaransa, katika Afrika Magharibi.
Alizaliwa nchini Ufaransa mwaka 1981 na jina lake halisi ni Stellio Gilles Robert Capo Chichi, akiwa na asili ya Benin.
Seba amejipatia umaarufu kupitia kampeni dhidi ya kile anachokiita “ukoloni mpya”, hasa kupitia upinzani wake dhidi ya sarafu ya CFA na ushawishi wa kiuchumi wa Ufaransa barani Afrika.
Hivi sasa anazungumziwa sana baada ya kukamatwa nchini Afrika Kusini, ambapo aliripotiwa kushikiliwa kwa makosa ya uhamiaji huku pia akitafutwa na mamlaka ya Benin kwa tuhuma za “kuchochea uasi” baada ya kuunga mkono jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwaka 2025.
Aidha, amekuwa mtu mwenye utata mkubwa, akiwahi kukamatwa mara kadhaa katika nchi mbalimbali kwa tuhuma zinazohusiana na uchochezi na kauli tata za kisiasa.
Wafuasi wake wanamuona kama mtetezi wa uhuru wa Afrika, huku wakosoaji wakimlaumu kwa kueneza propaganda na misimamo mikali ya kisiasa.
Chanzo:BBC














