Watu wasiopungua 12 wameuawa na wengine tisa kujeruhiwa siku ya Jumanne jioni wakati watu waliokuwa na silaha waliposhambulia eneo la kitongoji duni la Cleveland, mashariki mwa jiji la Johannesburg, polisi wamesema siku ya Jumatano.
Polisi walisema katika taarifa kuwa wameanza kuwasaka washukiwa zaidi ya 10 kufuatia mashambulizi katika kitongoji duni cha Jumpers.
Haijulikani chanzo cha mashambulizi hayo ni nini.
Polisi wanasema washukiwa walifika eneo hilo wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Quantum rangi nyeupe, wakaingia kwenye eneo hilo kupitia njia mbili tofauti na kufyatua risasi sehemu kadhaa kabla ya kuondoka na gari hilo.
Afrika Kusini ina viwango vikubwa vya mauaji duniani, kwa wastani watu 60 kwa siku.

















