Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, amempandisha cheo mwanaye Sean Mnangagwa ndani ya Jeshi la Taifa la Zimbabwe (ZNA), hatua iliyozua mjadala mkubwa nchini humo.
Sean Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 39 na anayehudumu katika kikosi cha ulinzi wa rais, amepandishwa kutoka cheo cha Meja hadi Luteni Kanali.
Amehudumu katika jeshi tangu mwaka 2010, wakati baba yake akiwa Waziri wa Ulinzi chini ya utawala wa rais wa zamani Robert Mugabe.
Sean pia amepata mafunzo ya kijeshi katika nchi mbalimbali ikiwemo China, Urusi na Msumbiji.














