Mamlaka za Madagascar zimemkamata raia mmoja wa France kwa tuhuma za kuhusika katika mpango wa kuchochea machafuko ya kisiasa nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya usalama, mtuhumiwa anadaiwa kushirikiana na watu wa ndani kupanga mikakati ya kuvuruga utulivu wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha maandamano yasiyo halali.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na mawasiliano na mipango iliyolenga kuzua taharuki miongoni mwa wananchi, jambo lililochukuliwa kwa uzito mkubwa na serikali.
Mamlaka zimeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kulinda usalama wa taifa, hasa katika kipindi ambacho nchi inakabiliwa na changamoto za kisiasa na kiuchumi
Kwa upande mwingine, ubalozi wa France umeeleza kuwa unafuatilia kwa karibu tukio hilo na kuhakikisha haki za raia wake zinalindwa wakati wa mchakato wa kisheria,
Wachambuzi wanasema tukio hilo linaweza kuathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ikiwa halitashughulikiwa kwa uwazi na haki.
Chanzo:BBC News
















