Mwanaharakati wa Pan-Afrika Kemi Seba ataendelea kubaki kizuizini kufuatia kuahirishwa kwa kesi inayomkabili mahakamani.
Kwa mujibu wa taarifa, kikao cha kusikiliza kesi hiyo kiliahirishwa kutokana na sababu za kisheria na kiutawala, jambo lililosababisha kuchelewa kwa mchakato wa haki,
Kemi Seba, anayejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ushawishi wa nchi za Magharibi barani Afrika, amekuwa akivutia uungwaji mkono na ukosoaji kwa wakati mmoja.
Wafuasi wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake ni hatua ya kisiasa inayolenga kunyamazisha sauti yake, huku mamlaka zikisisitiza kuwa taratibu za sheria zinafuatwa kikamilifu,
Kesi hiyo inaendelea kufuatiliwa kwa karibu na mashirika ya haki za binadamu pamoja na wadau wa siasa barani Afrika.
Chanzo:Africanews














