Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Asaad Al Shaibani, amefanya ziara yake ya kwanza rasmi nchini Misri ambapo alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty.
Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hizo mbili, mazungumzo yao yalihusu kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kupanua ushirikiano wa pande mbili pamoja na kujadili maendeleo ya kikanda na kimataifa.
Misri imeeleza kuwa ziara hiyo inaashiria hatua mpya ya kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya Cairo na Damascus.
CHANZO: TRT Afrika
















