Afrika

Urusi kuisaidia Msumbiji kupambana na ugaidi

Uamuzi huo, unafuatia ombi lilitoka kwa Rais Daniel Francisco Chapo, mara baada ya kukutana na Waziri wa Mambo wa Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

Newstimehub

Newstimehub

9 Julai, 2026

33c705dc f60e 450d b416 1bd363948eca 1783618411262

Urusi imesema kuwa ipo tayari kuisaidia serikali ya Msumbiji kupambana na vitisho vya kigaidi nchini humo.

Uamuzi huo, unafuatia ombi lilitoka kwa Rais Daniel Francisco Chapo, mara baada ya kukutana na Waziri wa Mambo wa Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

“Kati ya mambo mengine ambayo tumejadiliana, ni mapambano dhidi ya ugaidi,” alisema Lavrov.

 “Urusi ipo tayari kuwasaidia marafiki zetu wa Msumbiji kutokomeza tatizo la ugaidi nchini Msumbiji.”

Lavrov aliwasili jijini Maputo siku ya Alhamisi, baada ya kuzitembela Ethiopia na Niger.