Michezo

Atletico Madrid na Arsenal Watoka Sare ya 1-1 Nusu Fainali.

Atletico Madrid na Arsenal wametoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana.

Newstimehub

Newstimehub

30 Aprili, 2026

Katika mechi kali ya nusu fainali ya UEFA Champions League iliyochezwa jana, Atletico Madrid ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa mkondo wa kwanza,Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika za mwisho za kipindi cha kwanza kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Viktor Gyokeres baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari. Hilo liliwapa faida ya kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili, Atletico Madrid walirudi kwa nguvu na kusawazisha bao kupitia penalti iliyofungwa na Julian Alvarez baada ya VAR kubaini mpira wa mkono kutoka kwa beki wa Arsenal.

Mchezo huo ulikuwa wa kiufundi zaidi kuliko ule wa PSG dhidi ya Bayern, huku kila timu ikijaribu kucheza kwa tahadhari. Atletico walionekana kuwa bora zaidi kipindi cha pili na walipata nafasi kadhaa za kufunga, ikiwemo mpira uliogonga mwamba wa lango,dakika za mwisho kulikuwa na utata mkubwa baada ya Arsenal kupewa penalti nyingine, lakini ikaondolewa na VAR, jambo lililosababisha malalamiko makubwa kutoka kwa benchi la ufundi la Arsenal.

Matokeo hayo yanaacha kila kitu wazi kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa London, ambapo mshindi ataingia fainali.

Chanzo:The Guardian