Manchester City imefuzu kucheza fainali ya kombe la FA Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Southampton katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Wembley.
Katika mchezo huo, Southampton walikuwa wa kwanza kufunga bao, lakini City walifanya comeback ya haraka katika dakika za mwisho.
Mabao ya Jeremy Doku na Nico Gonzalez yaliihakikishia City ushindi huo muhimu na kuwapeleka fainali kwa mara ya nne mfululizo.
Ushindi huo unaongeza matumaini ya Manchester City kutwaa taji hilo msimu huu huku wakiendelea kufanya vizuri katika mashindano ya ndani.
City sasa watakutana na mshindi kati ya Chelsea na Leeds United katika fainali inayotarajiwa kufanyika mwezi Mei 2026.
Chanzo:The Guardian














