Polisi nchini Kenya wamekamata chatu mwenye urefu wa futi 13 aliyekuwa amefichwa ndani ya boksi kama vipuri kwenye basi la abiria.
Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Nairobi na lilisimamishwa katika kituo cha mpaka cha Namanga kwa ukaguzi wa kawaida.
Kwa mujibu wa polisi, nyoka huyo alipatikana ndani ya boksi lililofichwa, na wahudumu wa basi hilo wamekamatwa huku uchunguzi ukiendelea.
Tukio hili linaonyesha ongezeko la visa vya uhalifu wa wanyamapori nchini Kenya, ambavyo kwa kawaida huhusisha meno ya tembo na faru.
CHANZO: TRT Afrika














