Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema hatuna sababu ya kutumia silaha za nyuklia dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa nguvu za kawaida za kijeshi tayari zimeleta matokeo makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika White House, Trump alisema: “Kwa nini nitumie silaha ya nyuklia wakati tayari tumewaangamiza bila kuitumia?”
Aliongeza kuwa silaha za nyuklia hazipaswi kutumiwa na taifa lolote, akisisitiza umuhimu wa kudhibiti matumizi yake duniani.
Kauli hiyo inakuja wakati mvutano wa kijeshi kati ya Marekani, Israel na Iran ukiendelea kuathiri usalama wa kikanda na kimataifa.














