Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaadhimisha miaka 10 tangu kifo cha mwanamuziki mashuhuri wa Afrika, Papa Wemba, aliyefariki Aprili 24, 2016 akiwa jukwaani wakati wa tamasha la FEMUA mjini Abidjan.
Papa Wemba, ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alijulikana kama “Mfalme wa Rumba Rock” na mmoja wa waanzilishi wa muziki wa kisasa wa Congo.
Alianza safari yake ya muziki katika bendi ya Zaiko Langa Langa kabla ya kuanzisha kundi lake maarufu la Viva La Musica, lililompa umaarufu mkubwa barani Afrika na duniani.
Katika kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo chake, mashabiki kote DRC na maeneo mengine wanafanya matamasha, maonesho ya filamu na mikusanyiko maalum kumuenzi gwiji huyo wa muziki.














