Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeishutumu Rwanda kwa kuua zaidi ya raia 1,500 mashariki mwa nchi hiyo tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba, katika mapigano mapya yanayohusishwa na waasi wa M23.
Kwa mujibu wa serikali ya DRC, mashambulizi hayo yalihusisha matumizi ya mabomu na droni, licha ya kuwepo kwa makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani mapema mwezi huo. Waasi wa M23 waliripotiwa kuteka mji wa Uvira, hali iliyosababisha maelfu ya raia kukimbilia Burundi.
DRC imeitaja hali hiyo kama uchokozi wa wazi kutoka Rwanda, tuhuma ambazo Kigali imekanusha. Wakati huohuo, Umoja wa Mataifa unasema makumi ya maelfu ya watu wamekimbia makazi yao, huku mgogoro wa kibinadamu ukiendelea kuongezeka mashariki mwa DRC.
CHANZO: TRT Afrika














