Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limependekeza kufanya mabadiliko makubwa katika sheria ya kadi za njano kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Lengo la mabadiliko hayo ni kupunguza uwezekano wa wachezaji kukosa mechi muhimu kutokana na kukusanya kadi nyingi za njano katika hatua za awali za mashindano.
Kwa mujibu wa pendekezo hilo, kadi za njano zitafutwa baada ya hatua ya makundi kuelekea hatua ya mtoano, na pia baada ya robo fainali.
Mapendekezo hayo yanatarajiwa kujadiliwa rasmi katika kikao cha baraza la maamuzi la FIFA Aprili 28, 2026.
CHANZO: TRT Afrika














