Wizara ya Fedha ya Gabon imetangaza kusaini mpango wa nyongeza wa dola milioni 150 kutoka Benki ya Dunia, hatua inayoongeza jumla ya msaada wa taasisi hiyo kwa taifa hilo kufikia dola milioni 600.
Serikali ya Gabon imesema fedha hizo zitasaidia kufadhili miradi ya miundombinu ya msingi na kuimarisha usimamizi wa fedha za umma.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za nchi hiyo kuimarisha uchumi wake na kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika usimamizi wa fedha za serikali kwa miaka ya karibuni.
CHANZO: TRT Afrika














