Iran imesema ina “udhibiti thabiti” wa Ghuba ya Uajemi na Mlango Bahari wa Hormuz, ikisisitiza kuwa hakuna haja ya kuingilia kati kwa mataifa ya nje.
Kupitia taarifa ya jeshi la Khatam al-Anbiya, Iran ilieleza kuwa inasimamia njia hiyo muhimu kwa “uwezo na mamlaka kamili,” huku ikionya kuwa usalama utahakikishwa kwa njia zote zinazohitajika.
Pia ilisisitiza kuwa mataifa ya nje kama Marekani na Israel hayana haki ya kuingilia masuala ya usalama wa eneo hilo.
Hali katika mlango huo imekuwa tete tangu Machi, ambapo takribani mapipa milioni 20 ya mafuta hupita kila siku, na usumbufu wake umeongeza bei za mafuta duniani.
CHANZO: TRT Afrika














