Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahidi kuukomboa mji wa kimkakati wa Uvira baada ya kutekwa na waasi wa M23 mashariki mwa mkoa wa Kivu Kusini. Waziri wa Sheria Guillaume Ngefa amesema jeshi linaandaliwa upya kwa kushirikiana na vikosi vya washirika, huku mapigano mapya yakisababisha vifo, majeruhi na kuhamishwa kwa zaidi ya watu 200,000, kulingana na Umoja wa Mataifa.
CHANZO: TRT Afrika














