Takriban watu 10 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Urusi katika maeneo mbalimbali ya Ukraine.
Kwa mujibu wa mamlaka za Ukraine, mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na kujeruhi watu kadhaa, hali inayozidi kuongeza madhara ya vita vinavyoendelea.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa vikosi vya nchi yake vimefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa kulenga meli za kusafirisha mafuta na kituo cha kuhifadhi mafuta kinachotumiwa na Urusi.
Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kudhoofisha uwezo wa Urusi katika kusambaza rasilimali muhimu zinazotumika kuendeleza operesheni za kijeshi.
Wachambuzi wa kimataifa wanasema kuwa mashambulizi ya pande zote yanaendelea kuongeza mvutano na kuathiri usalama wa eneo hilo, huku juhudi za kidiplomasia za kumaliza vita zikiendelea kukabiliwa na changamoto.
Chanzu:BBC World














