Ulimwengu

Mlipuko wa volcano waua 3 nchini Indonesia, wengine 20 hawajulikani walipo

Watu watatu wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa volkano ya Mlima Dukono kwenye kisiwa cha Halmahera katika jimbo la North Maluku nchini Indonesia, huku wengine 20 hawajulikani walipo.

Newstimehub

Newstimehub

8 Mei, 2026

7d9f2a8e9d7ef512801abf53f41ebf6de175e70fb6b20d4452d5e9bfd1891067

Serikali ya Indonesia imesema imepeleka waokoaji ili kuwahamisha wapanda milima waliokwama kutokana na mlipuko huo.

Shirika la habari la Detik nchini humo limemnukuu Erlichson Pasaribu ambae ni afisa wa polisi akisema kuwa kati ya watu watatu waliofariki, mmoja ni raia wa kigeni.

Volkano hiyo ililipuka majira ya saa 1:41 usiku wa kuamkia Ijumaa (1041GMT Alhamisi), ikitoa wingu kubwa la moshi lililofika umbali wa takribani kilomita 10 angani.

Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Maafa la Indonesia (BNPB) lilisema: “Kuna taarifa za watalii wawili wanaoshukiwa kufariki katika tukio lililotokea eneo la Mlima Dukono.”