Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameonya kuwa operesheni za kijeshi za Israel katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati zinaongeza hatari ya kuzuka kwa mzozo mkubwa wa kikanda.
Akizungumza mjini Ankara wakati wa hafla ya iftar, Erdogan alisema hatua hizo zinaenea kutoka Gaza hadi Lebanon, Yemen na Iran.
Alisisitiza kuwa hali hiyo inaathiri raia wasio na hatia na kuongeza mvutano katika eneo hilo.
CHANZO: TRT Afrika

















