Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imekiri kuwa watu 518 walipoteza maisha katika vurugu hizo nchini Tanzania.
Ripoti hiyo iliwasilishwa na Mohamed Chande Othman kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifo hivyo vimeacha athari kubwa kwa familia, ikiwa ni pamoja na changamoto za kiuchumi na kuongezeka kwa utegemezi katika jamii.
Jaji Mkuu Mstaafu alisema idadi hiyo huenda isiwe ya mwisho kwani baadhi ya waathirika walitibiwa katika vituo binafsi bila kurekodiwa rasmi.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kutoa takwimu rasmi kuhusu idadi ya waliopoteza maisha katika tukio hilo.
CHANZO: TRT Afrika














