Serikali ya Ghana imewafukuza raia watatu wa Israel kama hatua ya kujibu madai ya kunyanyaswa kwa raia wake saba, wakiwemo wabunge, katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion nchini Israel. Waghana hao walizuiliwa bila maelezo na baadaye kuachiwa, huku watatu wakirudishwa nyumbani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana ilimwita Kaimu Balozi wa Israel kutafuta suluhu, ikisisitiza kuwa raia wake wanastahili heshima kama ilivyo kwa wageni wa nchi hiyo. Serikali ya Ghana ililaani vikali tukio hilo kabla ya kuchukua hatua ya kuwafukuza Waisraeli hao.
CHANZO: TRT Afrika














