Afrika

Serikali ya Kenya yapandisha tena bei ya mafuta

Serikali ya Kenya kupitia Mamlaka ya Kudhibiti Mafuta na Nishati (EPRA), imetangaza tena kupandisha bei ya mafuta kwa asilimia 23.5.

Newstimehub

Newstimehub

14 Mei, 2026

35556e168c9ec8b2ddd30a09e29855c8824d9991ab0f421ee8417422b58d3566

Serikali ya Kenya kupitia Mamlaka ya Kudhibiti Mafuta na Nishati (EPRA), imetangaza tena kupandisha bei ya mafuta kwa asilimia 23.5 baada ya kupandisha kwa asilimia 24.2 mwezi uliopiya.

Katika bei mpya zilizotangazwa, lita moja ya petroli jijini Nairobi sasa itauzwa kwa shilingi 214.25 za Kenya kutoka takriban shilingi 207.

Dizeli imepanda kwa kiwango kikubwa zaidi kutoka shilingi 196.63 hadi shilingi 242.92 kwa lita, kiwango kinachotajwa kuwa cha juu zaidi katika historia ya nchi hiyo. Hata hivyo, bei ya mafuta ya taa imebaki kuwa shilingi 152.78 kwa lita.

EPRA imesema ongezeko hilo limechangiwa na uhaba wa mafuta ghafi katika soko la dunia pamoja na kupanda kwa gharama za nishati kufuatia mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati. Kenya inaagiza karibu mafuta yake yote kutoka mataifa ya Ghuba kupitia mikataba ya serikali kwa serikali, hali inayofanya nchi hiyo kuathirika moja kwa moja na mabadiliko ya bei katika soko la kimataifa.