Sudan yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na UAE

Sudan imeitaja UAE kama ‘taifa la uchokozi,’ huku taifa hilo la Ghuba likikanusha madai ya kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF

Newstimehub

Newstimehub

6 Mei, 2025

burhan

Siku ya Jumanne Sudan imesitisha ushirikiano wa kidiplomasia na UAE na kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Abu Dhabi.

Katika taarifa, Baraza la Usalama na Ulinzi la Sudan limeitaja UAE kama “taifa la uchokozi,” na kuishtumu nchi hiyo ya Ghuba kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF.

“Dunia nzima imeshuhudia, kwa zaidi ya miaka miwili, UAE imefanya uhalifu dhidi ya uhuru wa Sudan, na mipaka yake, na usalama wa raia wake,” baraza hilo limesema.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuitupilia mbali kesi ya Sudan ya kudai kuwa UAE “inahusika na mauaji ya halaiki” katika mkoa wa Darfur magharibi kutokana madai ya kuwasaidia RSF, madai ambayo UAE inakanusha.

UAE haijasema chochote kuhusu uamuzi huo wa Sudan.

​​​​​​​