Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki, Abdulkadir Uraloğlu, amesema nchi hiyo haina changamoto yoyote ya usambazaji wa mafuta ya ndege kwa sasa.
Akizungumza baada ya mkutano wa Chemba ya Viwanda ya Istanbul, waziri huyo alieleza kuwa licha ya bei ya mafuta ghafi kupanda kwa zaidi ya asilimia 50, bei ya mafuta ya ndege imeongezeka zaidi ya mara mbili katika soko la kimataifa.
Aidha, alithibitisha kuwa ndege ya Pegasus Airlines iliyokuwa imekwama nchini Iran imerejea Uturuki, huku juhudi zikiendelea kurudisha ndege ya Turkish Airlines.
Safari za ndege kuelekea baadhi ya nchi za kikanda zimeghairiwa kutokana na kufungwa kwa anga, huku serikali ikiweka usalama wa abiria kuwa kipaumbele kikuu.
CHANZO: TRT Afrika














