Wanajeshi wa Nigeria wamewaua magaidi wasiopungua 20 katika operesheni iliyofanyika katika jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi katika kanda hiyo Sani Uba, wanajeshi walifanikiwa kuzuia jaribio la magaidi kuvamia kambi ya jeshi ya Goniri usiku wa kuamkia Jumanne.
Uba alisema katika mapigano hayo kamanda mmoja wa kundi la magaidi, aliyefahamika kwa jina la Abu Yusu Munzir wa Dursula, aliuawa pamoja na wapiganaji wengine.
Hata hivyo, baadhi ya wanajeshi walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo.
CHANZO: TRT Afrika














