Afrika Ajenda

Zaidi ya Watu 30 Wahofiwa Kufa Maji Baada ya Boti Kuzama Uganda

Ajali hiyo ilitokea Ziwa Nguse huku manusura wakihusisha tukio na kuzidishwa kwa abiria kupita uwezo wa boti.

Newstimehub

Newstimehub

30 Aprili, 2026

746

Zaidi ya watu 30 wanahofiwa kupoteza maisha nchini Uganda baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Nguse usiku wa Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, watu hao walikuwa wakirejea kutoka msitu wa Bugoma walikokwenda kuvuna mkaa kabla ya ajali hiyo kutokea katika kijiji cha Kyaleni, Manispaa ya Pachwa.

Msemaji wa Polisi wa eneo la Albertine, Julius Hakiiza, amesema hadi sasa mwili mmoja umeopolewa huku juhudi za uokoaji na utafutaji zikiendelea.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa boti hiyo huenda ilizidiwa uwezo baada ya kubeba watu wengi kuliko kiwango kinachoruhusiwa.

CHANZO: TRT Afrika