Afrika

Mkuu wa Exxon alitaka hakikisho la usalama kwa mradi wa gesi kutoka kwa rais wa Msumbiji

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Exxon, Darren Woods alitaka kuhakikishiwa usalama na rais wa Msumbiji Daniel Chapo kwa mradi wa gesi wa dola bilioni 30 kabla ya kuruhusu mpango huo kuendelea.

Newstimehub

Newstimehub

30 Septemba, 2025

2c2b1ce3e1c43e66e007001af8d4200bfe6452f781b341a041884961f72758c9

Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Exxon Darren Woods alieleza wasiwasi wake kuhusu hatari ya kundi la waasi katika eneo la kaskazini mashariki la Cabo Delgado, ambapo Exxon inapanga kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha gesi barani Afrika, ripoti ilisema, ikinukuu vyanzo vinavyofahamu mazungumzo hayo.

Wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Islamic State walianzisha uasi katika mkoa wa Cabo Delgado wenye utajiri mkubwa wa gesi mwaka 2017, na kuwaua maelfu ya raia, kutatiza maisha ya watu na kulazimisha maelfu wengine kuhama makazi yao, kulingana na mashirika ya misaada. Uasi huo umetatiza miradi ya nishati yenye thamani ya mabilioni ya madola.

Woods na Chapo pia walijadilli mipango ya TotalEnergies kuanzisha tena mradi wao wa gesi katika kiwanda cha karibu.

TotalEnergies ilikuwa imesitisha mradi huo 2021 baada ya wapiganaji kuvamia mji wa kaskazini wa Palma, kituo muhimu karibu na panapochimbwa gesi.