Ajenda Afrika

Watu 14 Wafariki Katika Ajali ya Ndege Karibu na Juba, Sudan Kusini

Ndege ndogo yaanguka dakika chache baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba.

Newstimehub

Newstimehub

27 Aprili, 2026

714

Takriban watu 14 wamepoteza maisha baada ya ndege ndogo kuanguka karibu na mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usalama wa Anga ya Sudan Kusini, ndege hiyo aina ya Cessna iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba majira ya saa moja na robo asubuhi kabla ya kuanguka umbali wa kilomita 20 kutoka jiji hilo.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa hali mbaya ya hewa na uoni hafifu huenda vilichangia ajali hiyo.

Waliofariki ni raia 12 wa Sudan Kusini pamoja na Wakenya wawili, huku miili ya waathirika ikielezwa kuungua vibaya kutokana na ajali hiyo.

CHANZO: TRT Afrika