Ajenda Afrika Mazingira

Tahadhari ya Hali ya Hewa: Mvua Kubwa Zatarajiwa Katika Mikoa 20 Tanzania

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa onyo la mvua kubwa zitakazonyesha katika mikoa 20 ya nchi.

Newstimehub

Newstimehub

29 Desemba, 2025

218

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa onyo la mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika mikoa 20 nchini, hali inayoweza kusababisha athari mbalimbali kwa jamii na shughuli za kila siku.

Kwa mujibu wa TMA, mikoa itakayokumbwa na mvua hizo ni pamoja na Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe na Morogoro. Mikoa mingine iliyo kwenye tahadhari ni Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Pwani ikiwemo Kisiwa cha Mafia, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imesema mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi na kuvuruga shughuli za kijamii na kiuchumi.

Wananchi, hususan wanaoishi katika maeneo yenye hatari, wametakiwa kuchukua tahadhari mapema na kuendelea kufuatilia taarifa rasmi zitakazotolewa na mamlaka husika.

CHANZO: TRT Afrika