Serikali ya Sudan imesema watu wasiopungua 17 wameuawa baada ya shambulio la ndege isiyokuwa na rubani kulenga kijiji cha Shukeiri katika jimbo la White Nile.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, shambulio hilo lilifanywa na wapiganaji wa RSF na lilisababisha vifo vya raia kadhaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Serikali imeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza wapendwa wao.
Maafisa pia wameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya RSF kutokana na mashambulizi hayo.
CHANZO: TRT Afrika














