Mahakama nchini Kenya imemhukumu raia wa China, Zhang Kequn, kulipa faini ya shilingi milioni 1 au kutumikia kifungo cha miezi 12 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha mchwa hai kinyume cha sheria.
Zhang alikamatwa mwezi Machi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport akiwa na zaidi ya mchwa 2,200, akijaribu kuwapeleka nje ya nchi.
Mahakama ilisema kuwa adhabu kali ni muhimu ili kukomesha vitendo kama hivyo vinavyozidi kuongezeka.
CHANZO: TRT Afrika














