Afrika

Nigeria Yaanzisha Mahakama ya Kijeshi Kuhusu Mpango wa Mapinduzi wa 2025

Jeshi la Nigeria limeanzisha court martial kuwafikisha mahakamani wanajeshi wanaotuhumiwa kupanga mapinduzi.

Newstimehub

Newstimehub

24 Aprili, 2026

400x225 cmsv2 9a2edbd2 c7f0 55a3 8713 cb9a01e9b698 9734970

Jeshi la Nigeria limeanzisha rasmi mahakama ya kijeshi (court martial) kuwashughulikia zaidi ya wanajeshi 30 wanaotuhumiwa kuhusika katika mpango wa mapinduzi uliodaiwa kufanyika mwaka 2025.

Kwa mujibu wa mamlaka za ulinzi, jumla ya wanajeshi 36 wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya uasi (mutiny) na jaribio la kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Majaji wa mahakama hiyo waliapishwa rasmi, huku kesi zikitarajiwa kuendeshwa kwa siri (closed doors) kutokana na unyeti wa suala hilo la usalama wa taifa.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali ya Nigeria kukabiliana na kile ilichokiita jaribio hatari ambalo lingeweza kumaliza utawala wa kidemokrasia uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Wakati huo huo, baadhi ya washukiwa raia tayari wamefikishwa katika mahakama za kiraia na kushtakiwa kwa uhaini na ugaidi, huku wakikana mashtaka hayo.

Chanzo:Africanews