Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema matamshi ya Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen kuhusu Uturuki yalikuwa ya kusikitisha, akiongeza kuwa suala hilo tayari limejadiliwa kupitia njia za kidiplomasia.
Akizungumza Ijumaa katika Chuo Kikuu cha Oxford, Fidan alisema Ankara ilichukua hatua za haraka za kidiplomasia baada ya kauli hizo na kwamba hali hiyo sasa imerekebishwa.
Von der Leyen alikuwa amesema mapema wiki hii kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa “kukamilisha bara la Ulaya ili lisije likaathiriwa na Russia, Uturuki au China,” kauli iliyozua hisia kali kutoka Ankara.
CHANZO: TRT Afrika














