Serikali ya China imetoa pongezi kwa baadhi ya mataifa ya Afrika baada ya kufuta vibali vya ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Taiwan, Lai Ching-te.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, hatua hiyo inaendana na kanuni ya “China moja,” ambayo inasisitiza kuwa Taiwan ni sehemu ya China na haipaswi kushiriki kama taifa huru katika majukwaa ya kimataifa.
Rais Lai alikuwa anatarajiwa kusafiri kwenda Eswatini kuhudhuria maadhimisho ya miaka 40 ya utawala wa Mfalme Mswati III pamoja na sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
Hata hivyo, safari hiyo ilikwama baada ya nchi kadhaa za Afrika, zikiwemo Seychelles, Mauritius na Madagascar, kufuta vibali vya ndege hiyo kupita katika anga zao.
China imesema hatua hiyo inaonyesha uungwaji mkono wa kimataifa kwa sera yake, huku ikisisitiza kuwa hakuna atakayeweza kuzuia “mwelekeo wa kihistoria” wa kuunganishwa kwa China.
CHANZO: TRT Afrika














